Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BODI YA MITIHANI YAVUNJWA

A77ac85be56f9f854851a225c1844ab5 BODI YA MITIHANI YAVUNJWA

Fri, 6 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

RAIS Lazarus Chakwera wa Malawi, ameagiza kuvunjwa kwa Bodi ya Mitihani ya nchi hiyo baada ya mitihani ya taifa ya mwaka nchini humo kusambaa katika mitandao ya kijamii kabla haijawafikia watahiniwa.

Mitihani ya sekondari nchini humo ilipangwa kuanza Oktoba 27, mwaka huu lakini imeahirishwa, hali iliyoleta ghasia na kusababisha wanafunzi kuandamana huku polisi wakitumia mabomu ya machozi kuwatawanya.

Ilielezwa kuwa, polisi wamewakamata takribani wanafunzi 38 na walimu watatu kwa kukutwa na karatasi sita za mitihani iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii

Chanzo: habarileo.co.tz