Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azimio wataka Ruto aombe radhi kutokana na matamshi yake kuhusu 'cartels'

Azimio Wataka Ruto Aombe Radhi Kutokana Na Matamshi Yake Kuhusu 'cartels' Azimio wataka Ruto aombe radhi kutokana na matamshi yake kuhusu 'cartels'

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: Radio Jambo

Wabunge wa kinara wa upinzani Raila Odinga sasa wanamtaka Rais William Ruto kuiomba nchi msamaha hadharani kwa madai ya kutishia wawekezaji.

Katika mkutano na waandishi wa habari bungeni, wabunge hao walimshambulia rais kwa kile walichokiita "kutishia wawekezaji".

Walikuwa kiongozi wa wengi katika seneti Stewart Madzayo, naibu wake Enoch Wambua na Seneta wa Migori Eddy Oketch.

"Inasikitisha sana kusikia Rais mzima akiwatishia wawekezaji nchini Kenya kwa kudai kwamba wamekamatwa, wamefukuzwa au kupelekwa mbinguni," Madzayo alisema.

Akizungumza Magharibi siku ya Jumapili, rais alizungumza kwa ukali kuhusu makampuni yanayokatisha tamaa mageuzi katika sekta ya sukari.

Rais aliwataka wawekezeji wote wa sukari ama waondoke Kenya, waende jela au waende mbinguni.

“Hawa wakora wote watoke. Hio kampuni ni ya wananchi na tutaipangia upya. Hakuna kesi tutaentertain hapo. Kesi watoe na wao wenyewe watoke,” Ruto alisema.

"Wakitaka kuniletea kisirani ama wahame Kenya ama nitawaweka jela ama wasafiri waende mbinguni," aliongeza.

Lakini Madzayo alisema madai ya vitisho vya Rais ni tishio la moja kwa moja kwa maisha, kitu alichokitaja kuwa ni kinyume cha katiba.

Je, hii ina maana kwamba ikiwa maoni yako ya kisiasa yatatofautiana na Rais basi una hatari ya kupungukiwa na hasira yake, kwa mfano, biashara zako kupachikwa jina la makampuni au kuishi kwa hofu kwa sababu maisha yako yanatishiwa!" alisema.

"Sisi kama Azimio, tunalaani matamshi kama haya yaliyotolewa na Rais kwa vile nchi hii ya Kidemokrasia inayotawaliwa na Utawala wa Sheria na athari mbaya za hisia kama hizo haziwezi kupitiwa kupita kiasi," aliongeza.

Chanzo: Radio Jambo