Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azimia baada ya kugundua nyumba aliyolipa kodi kwa miaka 15 ni ya mkewe

Martin Stampa Azimia baada ya kugundua nyumba aliyolipa kodi kwa miaka 15 ni ya mkewe

Mon, 8 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Martin Stampa; ni mwanaume ambaye amejikuta akizimia baada ya kugundua kuwa mke wake ndiye mwenye nyumba aliyokuwa analipia kodi kwa miaka 15.

Stampa ambaye ni raia wa Zambia amepatwa na masahibu hayo baada ya mke wake aitwaye Lushomo kugundua mumewe anamsaliti na mwanamke mwingine ambapo mume hakujivunga, akathibitisha kuchepuka na kumtambia mke wake huyo kuwa anatafuta mchepuko mwenye akili na atakayempa mawazo ya kimaendeleo zaidi kuliko yeye.

Baada ya kauli hiyo, mke wa Stampa akamwambia kuwa yeye ndiye hana akili maana amekaa kwenye nyumba hiyo kwa miaka 15 akilipa kodi zaidi ya laki 5 kwa mwezi bila kugundua kuwa alikuwa anamlipa mke wake ambaye ndiye mmiliki halisi wa nyumba.

Yaani kwa miaka yote hiyo mke ndiye alikuwa anapokea kodi na kumwambia mumewe anampelekea mwenye nyumba, kumbe nyumba ni yake.

Taarifa hiyo ilimshtua mno Stampa na alipooneshwa nyaraka za umiliki wa nyumba husika na kuona majina ya mke wake ndipo akaanguka na kuzimia na baada watu kumwagia maji akazinduka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live