Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Awapikia mawe watoto wake kupoza njaa

Mawe Moja 2 Awapikia mawe watoto wake kupoza njaa

Tue, 26 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mjane kutoka Mishomoroni eneo la Mlango Saba, kaunti ya Mombasa nchini Kenya ambaye aliwapikia mawe wanawe baada ya kukosa chakula ana sababu ya kutabasamu baada ya kupokea msaada kutoka kwa Wakenya.

Baada ya taarifa inayohusu familia hiyo Penina Bahati Kitsao kupatwa na masaibu, wengi walijitokeza na kumpa msaada wa chakula na pesa.

Akiwa mwingi wa furaha, mama huyo mwenye umri wa miaka 45 alisema watoto wake sasa wanaweza kupata mlo angalau mara tatu kwa siku, ambapo kwake ilisalia kuwa ndoto baada ya mumewe kuaga dunia 2019.

"Nina furaha isiyo na kifani. Siamini Wakenya wanaweza kuwa na roho safi hivi. Nimepokea simu kutoka kote nchini, wengi walitaka kujua jinsi wanaweza kunisaidia," mama huyo alifichua.



"Sijawahi kuwa na akaunti ya benki wala simu, hii ni mara yangu ya kwanza na ninaona ni kama muujiza," aliongeza.

Prisca alisema aliamua kumsaidia Penina baada ya kupata habari za kusikitisha kwamba aliwapikia mawe wanane waliokuwa na njaa.

Demu aapa hatawapa wazazi mahari akidai walimlazimishia ndoa Penina ana watoto wanane, kifungua mimba wake ana miaka 28 na kitinda mimba akiwa na miezi mitano.



Penina alisema kwamba mwanawe wa kiume mwenye umri wa miaka mitano ndiye alimshinikiza kupika mawe kwani alikuwa akilia njaa.

"Watoto wengine ni wazima na wanaelewa wakati hamna chakula, hata hivyo huyu wa kiume ni mgumu hawezi elewa kabisa, alishinda kulia hapa kutwa nzima na ndiposa akanifanya nikachukua hatua hiyo," aliongeza.

Charo Kaingu, 13, na mtoto wa tatu katika familia hiyo alielezea furaha yake kwamba hatimaye familia yeka inaweza kupata chakula kama familia zingine. Alidokeza kwamba ana imani siku moja ataweza kumsaidia mtu mwingine anayehitaji msaada jinsi nao walivyosaidiwa.



Penina aliwashukuru Wakenya kwa msaada waliompa na kuwaomba wahisani kuzidi kumsaidia ili apate suluhu la kudumu kuwalea wanawe. Namabari yake ya simu ni +254797850029.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live