Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Awamu ya pili ya kuondoka wanajeshi wa AU nchini Somalia imeanza

Somalia Somalia AU Awamu ya pili ya kuondoka wanajeshi wa AU nchini Somalia imeanza

Tue, 19 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Afrika umetangaza kuwa, awamu ya pili ya kuondoka kwa wanajeshi wa umoja huo kutoka Somalia imeanza.

Taarifa ya Umoja wa Afrika imeeleza kuwa, kuondoka huko kunafuatia ratiba ya kukabidhi shughuli za usalama kwa mamlaka ya nchi hiyo, ambayo inapambana na washirika wa al-Qaida katika eneo la Afrika Mashariki yaanii kundi la wanamgambo wa al-Shabab lenye makao yake nchini Somalia.

Mwaka jana, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kauli moja liliidhinisha Ujumbe mpya wa Mpito wa Umoja wa Afrika nchini Somalia, unaojulikana kama ATMIS, kuwasaidia Wasomali hadi majeshi yao yatakapowajibika kikamilifu kwa usalama wa nchi hiyo mwishoni mwa mwaka 2024.

Afisa mmoja wa ngazii za juu wa Umoja wa Afrika ameziambia duru za habari kkwamba, awamu ya pili ya kuwaondoa askari 3,000 wa ATMIS nchini Somalia imeanza na inatarajiwa kukamilika kufikia mwishoni mwa mwezi huu wa Septemba.

Kikosi hicho ambacho hapo awali kilikuwa kinajulikana kama AMISOM kiliondoa wanajeshi wake 2,000 wa kulinda amani nchini Somalia mapema mwaka huu. Wanamgambo wa al-Shabab wa Somaliai

Juhudi za kujenga uwezo wa kuviwezesha vikosi vya usalama vya Somalia kuchukua jukumu kamili la usalama wa nchini mwao wakati ATMIS itakapoondoka kikamilifu nchini Somalia mwezi Disemba 2024 zinaendelea.

Hivi karibuni, Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia alisema lengo la operesheni za kijeshi zinazoendelea nchini humo ni kulitokomeza na kulisambaratisha kundi la kigaidi la al-Shabaab katika kipindi cha miezi mitano ijayo.

Somalia imekuwa katika vita na mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la al-Shaabab lilioasisiwa mwanzoni mwaka mwaka 2004, na ambalo limetangaza kuwa na mfungamano na mtandao wa al-Qaeda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live