Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Avamia benki na kuvua nguo akilalamikia kupotea kwa KSh78k kwenye akaunti yake

C568d6087ea3146b Avamia benki na kuvua nguo akilalamikia kupotea kwa KSh78k kwenye akaunti yake

Wed, 26 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Mwanamume mmoja Mnigeria ameonyesha ghadhabu zake baada ya benki kumkata pesa kimakosa akisema suala hilo lilikosa kutatuliwa

- Akiwa kwenye benki hiyo, mwanamume huyo alivua nguo zake akishtumu kitendo hicho akisema alidhania benki ni mahali salama kuweka pesa zake

- Huku watu wakijaribu kumtuliza, jamaa huyo aliongezea kuwa hataruhusu shughuli zozote kuendelea hadi pesa zake zitakaporejeshwa

Video ya mwanamume mmoja Mnigeria akivuruga shughuli za benki kwa madai ya kutoweka kwa KSh 78,613 katika akaunti yake imeibua hisia mseto mtandaoni.

Akipakia video hiyo kwenye Twitter, jamaa Mnigeria kwa jina Gbemi Dennis alisema malalamishi ya mwanamume huyo yamekosa kushugulikiwa kwa mwezi mmoja sasa.

Katika video hiyo fupi, baba huyo ambaye alikuwa ameandamana pamoja na wanawe alisema walifukuzwa shuleni na hakuna pesa za kuwalipia karo.

Aliongezea kuwa amekuwa akiwasilisha malalamishi yake katika benki hiyo lakini juhudi zake ziliambulia patupu.

Mlinzi wa benki hiyo alijaribu kumtuliza bila kufaulu kisha alivamia ofisi moja ya benki hiyo na kuanza kuvua nguo zake akisema hataruhusu shughuli zozote kuendelea hadi pesa zake zitakaporejeshwa.



Huku wengine wakisema benki za Nigeria zinatakiwa kuboresha huduma zao za kutatua malalamishi, baadhi walihoji kuwa mwanamume huyo huenda ndiye wa kulaumiwa kwa sababu ya kadi yake.

@Bunda_lurvah alisema: "Mimi naweka pesa zangu benki kwa hivyo ziko salama. Mbona pesa zangu ziondoke kwenye akaunti yangu bila kujua na wakose kufanya chochote.Angalia vile huyo mwanamke hajali"

@MrTifey: "Unatakiwa kufahamu vyema tatizo kabla ya kuzua lawama. Huenda pesa zilitolewa kwenye akaunti yake kwa sababu ya kutoa taarifa za kadi yake ama sababu zingine nyingi."

@Sby107: "Kiburi cha baadhi ya wafanyakazi hunikera... Tazama vile yule mwanamke amempuuza. Mteja wenyu??? Nigeria ina matatizo kila mahali endapo Dangote atakwenda hapo kulalamika wote watakimbia kila mahali kumsaidia. Watu feki kila mahali."

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke