Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aussems amsotesha benchi Mbongo

Aussems+pic Aussems amsotesha benchi Mbongo

Mon, 2 Nov 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

KIUNGO mwenye asili ya Tanzania, Wiseman Maluleke ameendelea kusoteshwa benchi kwenye kikosi chake kipya cha Black Leopards huku wakikumbana na kipigo cha pili mfululizo msimu huu.

Wiseman ambaye wiki chache zilizopita alikuwa Tanzania ambako ni nyumbani kwa mzazi wake mmoja (mama), amejikuta katika wakati mgumu wa kupata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza cha Black Leopards tangu ajiunge na timu hiyo akitokea Polokwane City.

Black Leopards iliuanza msimu huu wa Ligi Kuu Afrika Kusini kwa kucheza mchezo wao wa kwanza dhidi ya SuperSport United na kupokea kichapo cha mabao 2-0 kabla ya kuchezea kingine cha mabao 3-1 dhidi ya Baroka aliyowahi kuichezea Abdi Banda.

Katika michezo yote hiyo miwili, kiungo huyo ameishia kukaa kwenye orodha ya wachezaji wa akiba.

Wiseman ana imani kuwa wakati wake ukifika kocha wa kikosi hicho, Patrick Aussems ambaye aliwahi kuinoa Simba ya Ligi Kuu Tanzania Bara, atakuwa akimpa nafasi ya kucheza mara kwa mara.

“Mwalimu bado ni mgeni na mimi pia ni mgeni nadhani atakuwa akiniona taratibu mazoezini sina hofu juu ya nafasi kwa sababu naamini kila kitu kitakuwa sawa hivi karibuni,” alisema.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz