Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Auawa na mamba baada ya kukiuka kujikinga na corona nyumbani

100444 Pic+rwanda Auawa na mamba baada ya kukiuka kujikinga na corona nyumbani

Sat, 28 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Rwanda. Mwanamume mmoja nchini hapa ambaye alikiuka amri ya kukaa nyumbani kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona, amefariki dunia baada ya kuuawa na mamba alipokwenda kuvua samaki.

Rwanda ambayo ina wagonjwa 41 iliwaambia wananchi wakae nyumbani kuepuka maambukizi. Meya wa Wilaya ya Kamonyi Kusini mwa Rwanda Alice Kayitesi, aliiambia BBC kuwa: “Alikuwa amekiuka sheria ya kukaa nyumbani, ni miongoni mwa watu wachache ambao hawaonyeshi ushirikiano katika sheria hii ya kukaa nyumbani ili kuzuia kusambaa kwa corona.”

Chanzo: mwananchi.co.tz