Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Auawa kwa kusababisha timu yake kufungwa

Flag Pallone Sports Equipment Uganda Ball 660x400 Auawa kwa kusababisha timu yake kufungwa

Tue, 13 Oct 2020 Chanzo: millardayo.com

Kutokea nchini Uganda Churchill Owaci (22) ameuawa na wachezaji wenzake kwa kufanya makosa yaliyopelekea kufungwa goli katika mechi ya kirafiki baina ya timu mbili za mtaani.

Mwenyekiti wa Kaunti Ndogo ya Agoro, Denis Onyon amesema, wachezaji wenzake walimpiga na baada ya mchezo Owaci alitaka kulipa kisasi kwa kumvuta mchezaji mwenzake kwenye baiskeli hali iliysababisha ugomvi zaidi.

Msemaji wa Polisi, ASP Jimmy Patrick Okema amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema wanawashikilia watu wawili kuhusiana na tukio hilo huku uchunguzi ukiendelea.

Chanzo: millardayo.com