Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atwoli aahidi kumsaidia kijana aliyemtafuta kupitia Twitter

7219d00ea10f3fed Atwoli aahidi kumsaidia kijana aliyemtafuta kupitia Twitter

Wed, 23 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Kijana kutoka Nanyuki alimtafuta Papa Atwoli kwenye twitter na kumuomba amsaidia kuendeleza ndoto yake ya masomoAlikubali ombi hilo na kuahidi kumtafuta kijana huyo ili ahakikishe anaendeleza masomo yake kama anavyotamaniAtwoli alielekea nchini Dubai ambapo Afrika na Asia zinafanya kikao kuhusu kufanya biashara kidigitaliKatibu wa COTU Francis Atwoli ameahidi kumsaidia kijana aliyemlilia kuhusu masaibu yake katika mtandao.

Kijana huyo alimwandikia Atwoli kwenye Twitter kuhusu masaibu ya familia yake ambayo yalikatiza ndoto yake ya masomo.

Alimtaka Papa Atwoli kumpa kazi yoyote ili aweze kuchuma mapeni ya kutosha kumuwezesha ajiunge na shule ili kuendeleza masomo yake.

"Jambo, mimi naitwa Maiyani kutoka Nanyuki. Nina miaka 25 na ninatoka familia isiyojiweza. Naomba unisaidie na kazi. Nilimaliza KCSE mwaka wa 2015 na kupata alama ya C. Tafadhali nisaidie na kazi ili nisaidie wazazi wangu," aliandika kijana hyo.

Atwoli aliahidi kuhakikisha kuwa Lekorei Maiyani anapata nafasi ya kuendeleza masomo yake ili kutimiza ndoto zake maishani.

"Naahidi kukupigia simu mara tu nikurudi nchini . Tutapanga vile utarudi shuleni ili uweze kuendelea na masomo," Atwoli alimwambia.

Upekuzi wa TUKO.co.ke ulionyesha mvulana huyo alikuwa ametafuta uhisani pia kupitia twitter awali lakini hakufaidika.

"Naomba usaidizi wenu. Naomba kujiunga na college nisomee plant operator na wazazi wangu hawana chochote.Mnisaidie na nitashukuru sana," aliandika kwenye twitter nyingine.

Atwoli Jumatano Juni 23 pia aliahidi kuwa alielekea nchini Dubai kwa mkutano kuhusu nafasi ya teknolojia kwenye biashara.

"Niko njiani kuelekea Dubai ambapo nitakuwa mwenyekiti wa mkutano kati ya Afrika na Uchina kuhusu nafasi ya dijitali kwenye biashara," alisema Mzee Atwoli.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 073248269.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke