Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atupwa jela miaka mitatu kwa uzamiaji

Hukumu Pc Data Atupwa jela miaka mitatu kwa uzamiaji

Tue, 12 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Raia wa Congo DR, Batumika Borauzima William (20) amehukumiwa kulipa faini ya Sh500, 000 au kwenda jela miaka mitatu baada ya kupatikana na hatia ya kuishi nchini bila kuwa na kibali.

 

William, amehukumiwa kifungo hicho jana April 11, 2022 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Hakimu Mkazi Mkuu, Rhoda Ngimbilanga, baada ya mshtakiwa kukiri shitaka lake.

Kabla ya kutoa adhabu hiyo, Mahakama ilitoa nafasi kwa mshitakiwa kujitetea kwanini asipewe adhabu. Hata hivyo mshtakiwa huyo alijitetea kuwa ni kosa lake la kwanza hivyo anaomba mahakama impunguzie adhabu.

"Mahakama imekutia hatiani kama ulivyoshtakiwa hiyo, utatakiwa kulipa faini ya Sh 500,000 na ukishindwa kulipa faini hii, basi utatumikia kifungo cha miaka mitatu jela"  amesema Hakimu Ngambilanga.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo ameshindwa kulipa faini hiyo na hivyo atatumikia kifungo hicho.

Awali, Mwendesha Mashitaka kutoka Idara ya Uhamiaji, Hadija Masoud  ameiomba mahakama itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine, wanaokaa nchini bila kuwa kibali.

Advertisement Akimsomea shitaka lake, wakili Masoud  amedai kuwa mshitakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo, April 8, 2022 katika Daraja la Tanzanite lililopo wilaya ya Ilala.

Inadaiwa siku hiyo ya tukio, mshitakiwa akiwa raia wa Congo DR alikutwa aliishi nchini bila kuwa kibali, wakati akijua kuwa ni kinyume cha sheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live