Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atupwa jela miaka 6 kwa kumtusi Rais Museveni

Edward Awebwa Edward Awebwa

Thu, 11 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama moja iliyopo Entebbe nchini Uganda imemuhukumu kifungo cha miaka sita jela TikToker mwenye umri wa miaka 24, Edward Awebwa baada ya Kijana huyo kuchapisha video fupi kwenye akaunti yake ya TikTok akimtusi na kumkashfu Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Mke wa Rais, Janet Museveni, na Mtoto wao Jenerali Muhoozi Kainerugaba.

Katika video hiyo, Awebwa amesikika akitoa matamshi ya kikabila na kutumia lugha chafu ambayo ilivuruga amani ya Familia ya Rais Museveni.

Nyaraka za Mahakama zinaonesha kuwa Awebwa alitenda makosa hayo kati ya February na March 2024 ambapo alifikishwa mbele ya Mahakama Jumatano July 10, 2024 na kukiri mashtaka ya matamshi ya chuki.

Hakimu Mkuu Mfawidhi Stellah-Maris Amabilisi akitoa uamuzi huo amesisitiza kuwa kiwango cha juu cha heshima na utu kinapaswa kutolewa kwa Rais, Mke wa Rais na Mtotoo wao na kwamba Mahakama ina wajibu wa kuhakikisha makosa ya aina hiyo yanadhibitiwa.

Awebwa ameshtakiwa chini ya sheria ya matumizi mabaya ya kompyuta na kupelekwa gereza la juu la Kigo Nchini humo kutumikia kifungo chake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live