Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atupwa jela miaka 15 kwa ku-fake CV

Daniel Mthimkhulu Daniel Mthimkhulu

Thu, 5 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Daniel Mthimkhulu, alidanganya kuwa na Shahada ya Uhandisi wa Mitambo kutoka Chuo Kikuu cha Witwatersrand na Shahada ya Uzamivu (PhD) kutoka Chuo Kikuu cha Ujerumani.

Aliajiriwa na Shirika la Reli la Abiria (#PRASA) mwaka 2000 na kupanda Cheo hadi nafasi ya Mkuu wa Uhandisi huku akitumia CV yake ya kughushi na kupokea mshahara wa Randi Milioni 2.8 (takriban Tsh. 425,654,320) kwa Mwaka.

Akiwa ameajiriwa PRASA, alighushi Barua ya Ofa ya Kazi kutoka Kampuni ya Ujerumani, hatua ambayo ilimfanya apandishwe mshahara ili Kampuni hiyo isimpoteze.

Anatajwa kuhusika kwenye mpango wa kununua treni mpya zenye thamani ya Randi Milioni 600 (takriban Tsh. Bilioni 91) kutoka Hispania, ambazo hazikuweza kutumika Nchini humo kutokana na kuwa na urefu wa juu kuliko viwango vinavyohitajika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live