Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atumbukia mtoni na kufariki akiwakimbia polisi

Mto Nile Pic.png Atumbukia mtoni na kufariki akiwakimbia polisi

Sat, 26 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke mmoja nchini Kenya amefariki baada ya kutumbukia mtoni alipokuwa akijaribu kuwakimbia polisi katika Kaunti ya Kakamega nchini Kenya.

Kwa mujibu wa tovuti ya Tuko ya nchini humo, Hellen Kadogo (35), alitumbukia kwenye Mto Yala na kuzama kufuatia msako wa wauza pombe haramu maarufu chang’aa (gongo) ambayo imepigwa marufuku katika eneo hilo.

"Alipowaona maafisa hao, alisema anaogopa kukamatwa na kwamba hakuwa na pesa za kuwapa, hivyo aliamua kutoroka," mzee mmoja katika eneo hilo alisema.

"Nilimsikia akijiuliza ni nini atafanya baada ya kusikia kuhusu msako huo. Alianguka mtoni huku akikimbia," mwanamke mwingine alisema.

Wakazi katika eneo hilo wamemlaumu chifu wa eneo hilo kwa kufanya vitendo vya kuwanyanyasa, walieleza kuwa kifo cha mwanamke huyo kimesababishwa na ‘utemi’ wa chifu huy.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live