Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atuhumiwa kubaka mara baada ya kutangaza kugombea Urais

Mgombea Ubakaji Atuhumiwa kubaka mara baada ya kutangaza kugombea Urais

Thu, 19 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jaji wa mahakama moja nchini Senegal ameamuru kiongozi mashuhuri wa upinzani, Ousmane Sonko, kufika mahakamani hapo kujibu mashtaka kwa tuhuma za ubakaji. Hayo yalithibitishwa jana Jumatano na mawakili wa Sonko na mshtaki wake.

Umashuhuri wa kisiasa wa Sonko -- ambaye alishika nafasi ya tatu katika uchaguzi wa rais wa Senegal mwaka 2019 umepanda kwa kasi kutokana na umaarufu wake kati ya vijana na ametangaza nia ya kugombea urais mwaka 2024.

Sasa hivi lakini inaonekana amekwaa kisiki au ni katika kampeni za kumzima kisiasa baada ya mfanyakazi mmoja wa saluni kudai kuwa amebakwa na Sonko na jaji wa mahakama kutoa hukumu afike mahakamani kujibu tuhuma hizo.

Lakini Sonko, mwenye umri wa miaka 48 na ambaye ni mkaguzi wa zamani wa ushuru, amekanusha madai hayoi na kusema yeye ni muhanga wa njama za Rais Macky Sall. Amesema, mashtaka hayo ya ubakaji ni ya kupandikizwa na ni sehemu ya njama ya kumzuia asigombee urais mwaka 2024.

 Jumanne wiki hii, jaji wa mahakama ya Senegal alitia saini agizo la kupelekwa kesi ya Sonko katika mahakama ya uhalifu ili ajibu mashtaka ya uhalifu anaodaiwa kuufanya mwaka wa 2021, ikiwa ni pamoja na vitisho vya ubakaji na mauaji. 

Mmoja wa mawakili wa Sonko, Cheik Khoureyssi Ba naye alithibitisha hatua hiyo jana Jumatano na kusisitiza kuwa, agizo hilo lilikuwa na pingamizi ya kisheria na akasema timu ya wanasheria wa Sonko imeamua kukata rufaa.

Wafuasi wa Sonko wanapongeza juhudi zake za kuzungumzia ufisadi na ubaguzi wa kijamii, pamoja na kukashifu mtego wa kiuchumi na kisiasa wa makampuni ya kimataifa na ya mkoloni wa zamani wa Senegal, yaani Ufaransa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live