Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atimuliwa Bungeni kwa kugawa peremende

Permende Bungeni Atimuliwa Bungeni kwa kugawa peremende

Thu, 6 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Kenya siku ya Jumatano alifukuzwa kikaoni kwa siku moja baada ya kupatikana akifawanya peremende kwa wenzake wakati mjadala ulipokuwa ukiendelea.

Fatuma Gedi alisema "viwango vya sukari vilikuwa vimeshuka" baada ya kushiriki kikao kirefu.

Alikuwa ametuhumiwa na mbunge mwenzake Ndindi Nyoro kwamba alikuwa akigawanya pesa ndani ya ukimbi wa bunge.

Bw Nyoro aliombwa kuthibitisha madai yake ya hongo na kuzuiliwa kuhudhuria vikao kwa siku mbili baada ya kukosa kufanya hivyo.

Bi Gedi alizuiliwa kuhudhuria kikao kimoja kwa kosa la kugawanya bungeni.

Wabunge waliidhinisha marekebisho kadhaa katika mswada wa vyama vya siasa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live