Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Athari, faida mvua zinazoendelea kunyesha Kenya

Idadi Ya Vifo Kutokana Na Mafuriko Kenya Imeongezeka Athari, faida mvua zinazoendelea kunyesha Kenya

Thu, 30 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchini Kenya mvua kubwa inaendelea kusababisha maafa na uharibifu mkubwa wa mali, idadi ya watu waliofariki kutokana mafuriko hayo ikiwa ni zaidi ya watu 120.

Katika mtaa wa Bengala eneo la Junda jimbo la Mombasa, pwani ya Kenya wingu la huzuni limetanda hapa, nyumba iliyoporomoka na kumuuwa kijana mwenye wa umri wa miaka 22 wakati alipokuwa amelala usiku mvua ikinyesha.

Changawa Karisa ni mmoja wa jamaa ya marehemu.

“ile kelele ya kwamba amkeni, amkeni sasa wale wenzake walipotoka tukaitwa tukaambiwa kuwa hiyo nyumba imeanguka. Tukamfukua alikuwa amefunikwa na mchanga tukamtoa akiwa amefariki.” alisema Changawa Karisa ni mmoja wa jamaa ya marehemu.

Lakini licha ya maafa, mvua hiyo imeleta afueni kwa wakulima. Fedis Mbura ni mkulima wa mahindi na mboga.

“Kuna mafanikio tumepata lakini hiyo mafanikio ni mimea ambayo iko juu ya milima. Wakulima wamejaribu, tumepanda mahindi, tumepanda maharagwe.’’ alisema Fedis Mbura.

Mshirikishi katika shirika la msalaba mwekundu kaunti ya Mombasa, Aisha Al-Husseni amesema wanaendelea kutoa hamasa kwa jamii.

‘‘Watu wetu wameanza kuzungumza na familia ambayo wanaishi katika maeneo ya hatari ili wahamia kwa maeneo salama.’’ alieleza Aisha Al-Husseni.

Idadi ya watu waliokufa kutokana na mafuriko nchini Kenya imefikia 120.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live