Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu Philip Anyolo: Pelekeni ushoga wenu huko

Askofu Mkuu Philip Anyolo Askofu Mkuu Philip Anyolo.

Mon, 25 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Askofu Mkuu Philip Anyolo mnamo Jumamosi aliwapiga marufuku viongozi wa kidini jijini Nairobi akiwaonya dhidi ya kubariki wapenzi wa jinsia moja yaani mashoga na wasagaji.

Hatua hii inamaanisha Askofu Anyolo anachukua mtazamo tofauti na agizo la Papa Francis ambaye mnamo Jumatatu, aliwaruhusu kirasmi mapadre katika kanisa hilo kuwabariki wanandoa wa jinsia moja.

Kwenye agizo hilo, Papa alisema kuwa mapadre wanaweza kubariki watu walio kwenye uhusiano wa kimapenzi wa aina hiyo, ikiwa hafla hizo si sehemu ya ratiba rasmi ya kanisa hilo.

Lakini mnamo Jumamosi, Askofu Anyolo alipinga vikali agizo hilo, akisema kuwa linapinga maagizo ya Mungu kuhusu uhalisia na maana halisi ya ndoa nchini.

Wadadisi wanasema kuna uwezekano agizo hilo la Papa likapata pingamizi zaidi kutoka kwa mataifa tofauti barani Afrika, ambako kanisa hilo lina ufuasi mkubwa.

Polisi wachunguza kisa cha vijana 4 kuuawa Buruburu kwa...Manunuzi Krismasi: Wengi wakimbilia vibanda

Chanzo: www.tanzaniaweb.live