Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu Margaret Wanjiru Kumlipia Karo Mtahiniwa Bora wa Mtihani wa KCPE 2020

A9466c84dbb973f6 Askofu Margaret Wanjiru Kumlipia Karo Mtahiniwa Bora wa Mtihani wa KCPE 2020

Sat, 17 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Faith Mumo aliibuka mwanafunzi bora katika mtihani wa kitaifa wa darasa la nane, KCPE mwaka wa 2020

- Mwanafunzi huyo alijizolea alama 433 kwa jumla ya alama 500

- Babake alipoteza ajira Machi 2020 pindi mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya COVID-19 uliporipotiwa nchini

- Askofu Margaret Wanjiru amejitokeza na kuahidi kwamba atamlipia Faith karo ya muhula wa kwanza atakapojiunga na shule ya upili

Aliyekuwa mbunge wa Starehe Askofu Margaret Wanjiru ameahidi kumlipia karo ya shule ya muhula wa kwanza mwanafunzi aliyeibuka mshindi katika mtihani wa kitaifa wa darasa la nane, KCPE Faith Mumo.

Faith ambaye alikuwa mwanafunzi katika shule ya msingi ya Karimwaindu alijizolea alama ya 433 kwa jumla ya alama 500.

Babake Paul Mumo ambaye ni mhasibu, alisema alipoteza ajira mwezi Machi pindi tu mlipuko wa virusi vya COVID-19 uliporipotiwa nchini.

Mumo alisema, yeye pamoja na familia yake walilazimika kuhamia mashinani kwa sababu hawangeweza kumudu maisha ghali ya jiji.

" Nashukuru kwamba Faith ni msichana ambaye anapenda kusali, huwa anajiamini na ni mwenye bidii. Shule zilipofungwa Machi 2020 kwa ajili mlipuko wa virusi vya COVID-19, tulilazimika kuhamia mashinani kule Kagundo, Mwaka huo ulikuwa mgumu sana kwa sababu pia mimi nilipoteza ajira.

" Mimi ni mhasibu na tangu Machi 2020 sijafanya kazi popote ila Faith alitia bidii masomoni," Mumo alisema.

Hali ngumu anayopitia ya kimaisha Mumo ndio imempelekea Askofu Wanjiru kutoa msaada wake kwa mwanafunzi huyo ili aweze kuendelea na masomo yake bila tatizo.

" Hongera Faith Mumo kwa kuibuka mwanafunzi bora katika mtihani wa kitaifa wa KCSE, ili kuwatia moyo na kuwahamasisha wasichana wengi kusoma, nimejitolea kumlipia Faith karo ya shule ya muhula wa kwanza anapojiandaa kujiunga na shule ya upili.

" Vile vile , ningependa kuwahimiza wazazi ambao watoto wao hawakufanya vema katika mtihani wa kitaifa wawashauri kwamba siri ya maisha sio kukata tamaa," Askofu Wanjiru alisema.

Faith aliambia vyombo vya habari kwamba angependa kuwa miongoni mwa madaktari shupavu wa neva ( Neurosurgeon) nchini baada ya kukamilisha masomo yake.

Akizungumza na wanahabari wa Citizen TV, Faith alisema amekuwa akichukizwa sana akitizama hali ambaye mwanabondia Conjestina Achieng' amekuwa akikabiliana nayo.

" Nikishajiunga na shule ya upili ya Kenya High ambayo imekuwa tamanio langu, ningependa kuwa daktari wa neva kwa sababu watu wengi wana matatizo ya kiakili na hali hii inanikera sana, singependa kumuona Conjestina akiwa katika hali hiyo," Faith alisema.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari zaidi hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke