Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari watoto wapigana wenyewe kwa wenyewe Sudan

Sudan Watoto Wanajeshiiiiiiii Askari watoto wapigana wenyewe kwa wenyewe Sudan

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watoto elfu 8 wanashiriki katika vita kati ya jeshi la Sudan na vikosi vya Rapid Support Forces (RSF).

Gazeti la Sudan Tribune limeandika kuwa: Tangu vita kati ya jeshi la taifa na Vikosi vya Majibu ya Haraka (RSF) vilipoanza hapo tarehe 15 Aprili, watoto elfu 8 wameajiriwa kushiriki katika vita hivyo.

Takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) zinaonyesha kuwa, zaidi ya watoto 435 wameuawa katika mapigano kati ya jeshi la taifa na Rapid Support Forces, na zaidi ya wengine elfu 2,025 wamejeruhiwa.

Mwezi uliopita wa Septemba jeshi la Sudan lilitangaza kuwa askari watoto 230 walitekwa nyara katika mapigano na RSF, na kwamba 30 kati yao waliachiliwa huru na kukabidhiwa kwa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu.

Mwezi Septemba mwaka huu pia, Baraza la Ustawi wa Watoto liliiomba Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya Hague nchini Uholanzi kuwafungulia mashtaka na kuwaadhibu viongozi wa Rapid Support Forces (RSF) kwa kutumia watoto 6,000 katika vita hivyo. Baadhi ya watoto hao wamepoteza maisha vitani, na wengine wamejeruhiwa vibaya.

Wakati huo huo UNICEF imetangaza katika taarifa yake kwamba: Takriban watoto milioni 19 wa Sudan hawaendi shule, na kwamba iwapo vita kati ya jeshi na RSF havitahitimishwa, inatazamiwa kwamba milango ya shule haitafunguliwa kwa watoto wa Sudan katika mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live