Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari wapewa mikate na maziwa kama 'menyu' ya uchaguzi

Ndinga Gari Polisi.jpeg Askari wapewa mikate na maziwa kama 'menyu' ya uchaguzi

Tue, 11 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ripoti mpya imefichua kwamba maafisa wa polisi waliolinda vifaa vya uchaguzi, siku ya mkesha wa uchaguzi mkuu na kushika doria walilishwa mkate na maziwa siku nzima

Ripoti hiyo halikadhalika ilifichua kwamba baadhi ya polisi walilazimika kutafuta mlo kwingineko, na kwa kutumia gharama yao.

Licha ya kutopewa chakula kinachofaa, maafisa hao walisimama kwa muda mrefu na kukosa usingizi kwa siku mbili huku wakitekeleza majukumu yao

Ripoti mpya imefichua kwamba maafisa wa polisi waliolinda vifaa vya uchaguzi, siku ya mkesha wa uchaguzi mkuu na kushika doria walilishwa mkate na maziwa siku nzima.

Ripoti hiyo iliyotolewa na Mamlaka ya Kutathimin Utendakazi wa Polisi (IPOA) inaonesha kuwa polisi walioshika doria maeneo mengine walipewa mlo mara moja au mara mbili kwa siku.

Ufichuzi huu unakwenda kinyume na ahadi zilizotolewa na tume Huri ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).

"Ingawaje IEBC ilikuwa imeahidi kuwa ingetoa mlo kwa maafisa wa polisi waliohusika kushika doria wakti wa uchaguzi, timu ya ukaguzi iligundua kwamba kuna maeneo ambayo polisi walikosa kupewa mlo inavyohitajika.

"Maslahi ya polisi waliotumwa wakati wa uchaguzi hayapewa kipaumbele kama ilivopendekezwa na mamlaka kwenye ripoti za awali za uchaguzi," ripoti hiyo ilisema.

Ripoti hiyo halikadhalika ilifichua kwamba baadhi ya polisi walilazimika kutafuta mlo kwingineko, na kwa kutumia gharama yao.

Licha ya kutopewa chakula kinachofaa, maafisa hao walisimama kwa muda mrefu na kukosa usingizi kwa siku mbili huku wakitekeleza majukumu yao.

IPOA ilisema kwamba maafisa hao kukosa kulala kwa siku mbili, kuliwafanya wakawa wachovu, na hilo lingehatarisha usalama wa maafisa hao waliojihami kwa silaha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live