Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari waliokuwa likizo waagizwa kurudi kazini haraka

Fb2b2f439c27ff66 Askari waliokuwa likizo waagizwa kurudi kazini haraka

Sat, 13 Nov 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Inspekta Jenerali wa polisi nchini Kenya, Hillary Mutyambai amewagiza maafisa wote waliokuwa likizoni kurudi kazini huku kukiwa na hali ya wasiwasi wa usalama kote nchini.

Mutyambai ameagiza maafisa wote waliokuwa likizo kurejea kazini kabla ya Novemba 15 Agizo hilo lilitolewa baada ya Rais Uhuru Kenyatta, kamanda mkuu wa vikosi vya jeshi, kutoa wito wa mashirika ya ulinzi na ujasusi kukaza kamba.

Jumanne, Novemba 5, maafisa wa upelelezi DCI waliahidi kutoa zawadi ya KSh 50 milioni kwa yeyote atakayetoa habari zitakazowezesha kukamatwa kwa washukiwa watano wa ugaidi

Mutyambai aliagiza maafisa wote waliokuwa wakifurahia likizo kurejea kazini kabla ya Novemba 15.

Agizo hilo lilitolewa baada ya Rais Uhuru Kenyatta, kamanda mkuu wa vikosi vya jeshi, kutoa wito wa mashirika ya ulinzi na ujasusi kukaza kamba kufuatia hali ya wasiwasi ya usalama Ukanda wa Afrika Mashariki.

Katika taarifa iliyotolewa na Afisi ya Msemaji wa Rais, Kanze Dena, kiongozi wa taifa aliagiza taasisi zote za ulinzi wa ndani kuwa macho kufuatia hali ya usalama katika eneo hilo.

"Mheshimiwa Rais Uhuru Kenyatta ameagiza taasisi za usalama wa ndani kuwa makini kufuatia hali ya usalama inayoendelea kuzua wasiwasi nchini" ilisoma taarifa ya Kanze.

Maagizo hayo ya Uhuru yanajiri wakati nchi ikiwa katika hali ya tahadhari na kuongeza wanajeshi wa Kenya katika mipaka ya Kenya na Somalia na Ethiopia.

Hali ya hatari ilitangazwa nchini Ethiopia, na Waziri Mkuu Abiy Ahmed alitoa wito kwa watu walio na uwezo kuchukua silaha wakati waasi wa Tigray wakipenya kuelekea mji mkuu, Addis Ababa.

Kulikuwa na hofu kwamba mzozo huo unaweza kusambaa hadi nchi jirani kama vile Kenya.

Nairobi ina uhusiano tete na Mogadishu kutokana na mzozo wa mpaka wa baharini, na madai ya kuingiliwa kwa kisiasa kunatishia utulivu wa eneo lote.

Mnamo Jumanne, Novemba 5, Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) iliahidi kutoa zawadi ya KSh 50 milioni kwa yeyote ambaye atatoa habari zitakazowezesha kukamatwa kwa washukiwa watano wa ugaidi.

DCI ilifahamisha umma kwamba washukiwa hao watano wamejihami na ni hatari.

Yeyote aliye na taarifa zozote kuhusu waliko apige simu ya bure 0800722203.

Miongoni mwao ni mfungwa wa zamani wa ugaidi Elgiva Bwire, ambaye aliachiliwa Alhamisi, Oktoba 28, kutoka gereza la Kamiti Maximum.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke