Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari waliofutwa kazi wapewa nafasi ya kujitetea

Polisi Zi 800x500 Askari waliofutwa kazi wapewa nafasi ya kujitetea

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya Tume ya Kitaifa ya Huduma za Polisi nchini kenya inayohusika na masuala ya Rufaa na Sheria (APLA), imeanza kusikiliza rufaa iliyowasilishwa na maafisa wa polisi waliofutwa kazi.

Tume hiyo inaskiza kesi hizo katika jitihada za kuondoa mrundiko wa kesi zilizowashilishwa kwa tume hiyo na maafisa wa polisi wa zamani.

Wakiongozwa na mwenyekiti wa APLA Kamishna Edwin Cheluget, alisema kuwa jopo hilo linapania kusikiliza rufaa za maafisa wa polisi wa zamani ambao walifutwa kazi kwa makosa mbalimbali ya kinidhamu.

Akizungumza katika makao makuu ya kitengo cha polisi cha K-9 Kanda ya Rift Valley, Oktoba 12, 2023, Cheluget alisema kuwa mpango huo unalenga maafisa wanaotoka South na North Rift.

Kulingana na Kamishna Cheluget, kusikilizwa kwa rufaa moja kwa moja ni sehemu ya juhudi za tume kuhakikisha kuwa hatua za kiutawala zinachukuliwa  kwa mujibu wa Kifungu 47 cha Katiba ya Kenya.

“Leo tuna vikao vya rufaa za maafisa wa zamani wa polisi wanaohitaji kusikilizwa na leo tuko hapa Nakuru. Hii ni mara ya kwanza tunafanya rufaa moja kwa moja, tunajaribu kuona kila afisa anapata fursa ya kusikilizwa kabla ya kesi yake kuamuliwa,” alisema.

Kulingana na Kamishna Cheluget, hatua hiyo ni tofauti na hapo awali ambapo maafisa waliofutwa walitakiwa kuwasilisha malalamishi yao kwa njia ya kutuma.

Alibainisha kuwa wanasikiliza rufaa za taaluma kadhaa zilizoletwa na maafisa wa Huduma ya Polisi wa Utawala, Huduma ya Kitaifa ya Polisi pamoja na maafisa wa Idara ya Upelelezi (DCI).

Tume hiyo pia itazuru Mombasa na Kisumu ili kujaribu kupunguza mrundiko wa kesi za rufaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live