Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari polisi apoteza bunduki mazingira ya kutatanisha

Askari Polisi Apoteza Bunduki Mazingira Ya Kutatanisha Askari polisi apoteza bunduki mazingira ya kutatanisha

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: Radio Jambo

Afisa wa polisi alikamatwa Alhamisi baada ya bunduki yake rasmi kupotea katika mazingira ya kutatanisha katika eneo la Mathare, Nairobi.

Polisi huyo alidai kuwa alikuwa ameacha bunduki yake ya Scorpion ikiwa na risasi 30 ndani ya nyumba yake na kwenda kununua dawa.

Hata hivyo, aliporudi alikuta nyumba imevunjwa na silaha haipo. Aliiacha silaha hiyo ndani ya nyumba hiyo na kwenda kwa mkemia kwa ajili ya kupata dawa na ndipo ikadaiwa kuwa tukio hilo la uvunjaji wa nyumba lilitokea.

Aliporejea, alidai kuwa alikuta nyumba yake ikiwa imevunjwa na kwamba bunduki na risasi hizo ziliibwa.

Simu yake ya mkononi pia iliibiwa. Nyumba ya jirani yake pia ilivunjwa lakini hakukuwa na kitu chochote kilichoibiwa kutoka hapo.

Polisi walifanya msako katika eneo hilo bila mafanikio.

Mkuu wa polisi wa Nairobi Adamson Bungei alisema wanachunguza tukio hilo.

Afisa huyo alizuiliwa huku uchunguzi ukiendelea.

Silaha hizo zikiibiwa, kwa kawaida hutumika katika kufanya uhalifu mjini.

Kesi za uhalifu wa kutumia silaha zimekuwa zikiongezeka huku kukiwa na wito wa kudhibiti hali hiyo na kupata silaha zinazotumika.

Maafisa zaidi wa polisi wametumwa katika mitaa mbalimbali ili kudhibiti magenge hayo.

Chanzo: Radio Jambo