Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari auawa na mkewe kwa kuchelewa kurudi nyumbani

IMG 20240404 WA0011 Askari auawa na mkewe kwa kuchelewa kurudi nyumbani

Sat, 6 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Huko Kiplombe nchini Kenya, Ofisa wa polisi wa kitengo maalum ameuawa kwa kuchomwa na panga na mkewe kisa kikidaiwa ni kuchelewa kurudi nyumbani.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, Ofisa huyo aliyefahamika kwa jina la Vincent Kipterim alishambuliwa kwa panga na mke wake aliyefahamika kwa jina la ZamZam Bashir (26) baada ya kufika nyumbani mishale ya saa 9 alfajiri, Jumanne ya Aprili 2, 2024.

Inaelezwa na mashuhuda kuwa baada ya Vincent kufika akiwa amechelewa kulizuka ugomvi mkubwa baina yao, ugomvi ambao ulisababisha Vincent kuchomwa na panga ambapo alikimbizwa Hospitali kwa matibabu lakini alifariki muda mchache baadae kutokana na majeraha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live