Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari ashambulia waombolezaji kwa risasi, 13 wafariki

Risasi Congo Waombolezaj.jpeg Askari ashambulia waombolezaji kwa risasi, 13 wafariki

Mon, 24 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa kutoka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zinasema kuwa, kumetokea tukio la kushangaza na la ajabu la kuuliwa kwa umati watu 13 waliokuwa kwenye maombolezo ya mwanawe usiku wa kuamkia jana Jumapili.

Taarifa hiyo inasema kuwa, askari mmoja wa Serikali amekurupuka ghafla na kuanza kuwapiga risasi watu waliokuwa kwenye maombolezo ya mtoto aliyefariki dunia mashariki mwa DRC.

Maeneo ya kati, mashariki na kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yamekumbwa na machafuko kwa zaidi ya miaka ishirini sasa. Kuna zaidi ya vikundi 120 vya waasi wenye silaha mashariki mwa nchi hiyo na kila kikundi kinajichukulia hatua mikononi kulinda maslahi yake binafsi.

Jeshi la DRC lilitangaza jana Jumapili kwamba, askari huyo aliufyatulia risasi umati wa waombolezaji Jumamosi usiku, na kuua takriban watu 13, wakiwemo watoto wadogo tisa.

DRC kuna makumi ya magenge ya waasi

Askari huyo ambaye ni kutoka kikosi cha jeshi la wanamaji la Kongo, aliwafyatua risasi watu waliohudhuria mazishi ya mwanawe wa kumzaa katika kijiji cha Nyakowa kwenye fukwe za Ziwa Albert katika jimbo la Ituri Mashariki.

Hadi tunaandika habari hii ilikuwa bado haijajulakina ni kwa nini askari huyo aliamua kuchukua hatua kama hiyo mbaya. Chifu wa kijiji hicho,

Oscar Baraka Mogowa amesema kuwa, anadhani sababu ya mwanajeshi huyo kufanya mauaji hayo ya umati ni kutokana na huzuni kubwa aliyoipata na hasira zilizomkubwa baada ya kuona kuwa mtoto wake amezikwa bila ya yeye kuwepo.

Kwa sasa maafisa husika wanamsaka askari huyo na wameanzisha uchunguzi wa kubaini ni katika mazingira gani tukio hilo la kutisha limetokea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live