Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari aliyeua ndugu watano azua gumzo Afrika Kusini

Ndlovu Nomia Rosemary Ndlovu, Mshitakiwa wa mauaji ya watu watano

Tue, 28 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesi ya mauaji inayomkabili Afisa Polisi wa kike nchini Afrika Kusini anayetuhumiwa kufanya mauaji ya watu watano wakiwemo ndugu zake wanne pamoja na mpenzi kwa madai ya kushinikiza kupata fedha ya bima imechukua taswira mpya nchini humo kufuatia matendo aliyoonesha Polisi huyo akiwa kizimbani.

Polisi huyo anaefahamika kwa jina la , Nomia Rosemary Ndlovu, mwenye miaka 46, alionekana akiwa anainua nyusi kwa dharau kizimbani hapo akiwa amevalia mavazi ya gharama na ya kumpendeza tofauti na watu walivyotarajia.

Askari huyo wa zamani aliyeheshimiwa, amewashangaza Waafrika Kusini kwa tabia alizofanya akiwa kortini, alionekana akiwa anavuta uso kwa dharau sambamba na kuonesha alama ya vidole kuashiria kuwa hajali kila kitu kipo shwari kwake mara tu kamera zinapo elekezwa kwake.

Inaelezwa kuwa mtuhumiwa huyo alitekeleza mauaji hayo kati ya mwaka 2012 na 2017, ambapo dada, binamu, mpwa, rafiki wa karibu, pamoja na mpenzi wake walikutwa wamefariki huku wakiwa na majeraha mengi mwilini.

Mpaka sasa polisi huyo ndiye mtuhumiwa pekee anayeshikiliwa na vyombo vya usalama nchini humo, huku ushaidi kuhusu kesi hiyo ukiwa umekamilika.

Hata hivyo Polisi huyo mara zote amekuwa akikataa kuhusika na mauaji hayo ya watu wake wa karibu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live