Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari afukuzwa kazi baada ya kupoteza fahamu kwa miezi 9

Polisi Kenya1 Polisi

Fri, 24 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa mmoja wa Polisi nchini Kenya, Reuben Kimutai Lel amefukuzwa kazi baada ya kupotea kazini kwa miezi tisa baadaye kurejea tena akidai kuwa alikuwa akipatiwa matibabu.

Kimutai alitangazwa kutoroka kazi huku mshahara wake ukisimamishwa baada ya juhudi za wenzake kumtafuta kwa miezi kadhaa bila kumpata. Juhudi zao za kumtafuta kupitia familia yake ambayo pia ilikua ikimtafuta hazikuzaa matunda.

Kimutai alishtakiwa bila kuwa mahakamani huku hati ya kukamatwa kwake ikitolewa na mahakama, hata hivyo kesi hiyo baadaye ilifutwa baada ya polisi kushindwa kumpata.

Baadaye ilibainika kwamba ofisa huyo alikuwa amelazwa hospitali akiwa amepoteza fahamu alikuwa ametoweka tangu Desemba mwaka jana hadi wiki iliyopita alipopata fahamu. Japokuwa hajarudisha kumbukumbu yake kabisa, aliweza kujitambulisha kwa jina na kujieleza alikuwa ofisa wa polisi na mara baada ya hapo shughuli ya kutafuta familia yake ikaanza.

Ofisa huyo alikuwa mhanga wa ajali ya barabarani iliyotokea jjijini Nairobi na alilazwa katika Hospitali Kuu ya Rufaa mnamo Desemba 21, kama mtu asiyejulikana. Hakuwa na stakabadhi zozote za kumtambulisha kama alikuwa akipatiwa matibabu. Imeripotiwa kwamba, anatarajiwa kurejeshwa kwenye orodha ya malipo ya huduma ya polisi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live