Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari Polisi watano mbaroni kwa kuomba rushwa ya Tsh mil 8.4

Rushwa123 Askari Polisi watano mbaroni kwa kuomba rushwa ya Tsh mil 8.4

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tume ya Maadili na Kupambana na Rushwa (EACC) imewakamata Maafisa 5 wa Kitengo cha Usalama Barabarani kwa tuhuma za kuomba Rushwa ya Tsh. Milioni 8.4 kutoka kwa Madereva katika Barabara Kuu ya Thinka - Garissa.

Kukamatwa kwao kunafuatia Malalamiko yaliyowasilishwa na mmoja wa Madereva kupitia (EACC) na kueleza kuwa mmoja wa Maafisa ho amekuwa akiwambia wakitoa kiasi hicho cha Fedha ataondoa mashtaka ya mmoja wa Madereva na kuachia mzigo walioukamata.

Mkurugenzi Mtendaji wa EACC, Twalib Mbarak ametoa wito wa kuharakishwa kwa mfumo wa Uongozaji Magari unaojiendesha wenyewe "Automatic Traffic Sytem" ili kudhibiti Rushwa Barabarani pamoja na kuongeza uadilifu na ufanisi wa Sheria za Trafiki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live