Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari 15 wauawa kwa mlipuko wa bomu

Burknadee 15 Wauawa Askari 15 wauawa kwa mlipuko wa bomu

Wed, 10 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Askari wasiopungua 15 wa jeshi la Burkina Faso wameuawa kaskazini ya nchi wakati gari lililowabeba lilipokanyaga viripuzi na kusababisha vifo vya askari kadhaa kabla ya mripuko wa pili kuua askari wengine waliokimbilia eneo la tukio kutoa msaada kwa wenzao.

Taarifa iliyotolewa na jeshi imesema, tukio hilo lilitokea jana katika barabara ya mashambani ya mkoa wa Bam ulioko kati-kaskazini ya nchi, ambako askari na raia wamekuwa wakilengwa kila mara na mashambulio ya makundi yanayobeba silaha.

Magaidi wenye mfungamano na makundi ya Al-Qaeda na ISIS wamekuwa wakiendesha harakati zao katika maeneo hayo tangu mwaka 2015.

Taarifa ya jeshi la Burkina Faso imeeleza kwamba, shambulio hilo la jana lilitokea wakati moja ya magari yaliyokuwa yakisindikiza askari lilipokanyaga viripuzi karibu na wilaya ya Namsiguiya mkoani Bam.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, wakati zoezi la uokoaji na utoaji msaada lilipokuwa likiendelea, kiripuzi cha pili, ambacho inaaminika kilikuwa kikiongozwa kutokea mbali kiliripuka na kuua askari wengine kadhaa.

Shambulio la jana limejiri katika muda wa chini ya wiki moja tangu wapiganaji wanaobeba silaha walipoua wanajeshi wanne na askari wengine tisa wa kiraia wa kujitolea katika shambulio jengine la kuvizia lililotokea katika mkoa huohuo wa Bam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live