Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Asilimia 40 ya wabunge wana vyeti feki, Moses Kuria Asema

E10d12a6539ddbe7 Asilimia 40 ya wabunge wana vyeti feki, Moses Kuria Asema

Sat, 17 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Kuria alishangaa ni kwa nini mgombea wa chama chake anasakwa kwa kuwa na vyeti feki

- Alisema hiyo ndiyo kawaida ya waheshimiwa na walio na stakabadhi halalai ni wachache

- Makachero kwa sasa wanamsaka Koimburi alipokosa kufika mahakamani kujibu mashtaka

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria amemtetea mgombea wa kiti cha ubunge katika uchaguzi mdogo wa Juja George Koimburi anayedaiwa kuwa na vyeti feki.

Kiomburi anadaiwa hana vyeti halali vya masomo ya kidato cha nne sawa na chuo kikuu ila alivyowasilisha kwa tume huru ya miapaka na uchaguzi (IEBC) ni feki.

Koimburi anawania kiti hicho kilichoachwa wazi na aliyekuwa Mbunge Francis Waititu maarufu kama Wakapee kwa tiketi ya chama cha Kuria, People's Empowerment Party (PEP).

Kuria alisema kinachoendelea ni mbinu za wapinzani wao Jubilee kwenye uchaguzi huo mdogo kuhangaisha mgombea wake.

Alisema Jubilee inahofia ushindani wa mgombea wake na hivyo kuanza kutumia asasi za serikali kuwapiga kisiasa.

Kulingana na Kuria, idadi kubwa ya waliochaguliwa wabuunge hawana stakabadhi halalai na kwa hivyo Koimburi anafaa kuachwa apambane na wapinzani wake kwenye debe.



"Asilimia kama 40 ya wabunge kwenye bunge hili la 12 wana stakabadhi feki, cheti pekee kilicho hallali ni kile cha kuendesha gari," alisema Kuria.

Mbunge huyo ambaye ni mkosoaji mkuu wa Rais Uhruu Kenyatta katika mkoa wa Kati amekuwa akiahidi kukipa chama cha Rais funzo kwenye uchaguzi huo mdogo.

IEBC imeratibu uchaguzi huo ufanyika Mei 18.

Mahakama ya Kiambu iliagiza OCS wa Kiambu kumkamata Koimburi alipokosa kufika mahakamani Aprili 14 kujibu mashtaka ya kuwa na vyeti feki.

Kulingana na kachero anayefuatilia kesi hiyo, DCI iliandikia tume ya mitihani humu nchini KNEC ambao walifutilia mbali cehti cha Koimburi cha shule ya upili.

Aidha hatua kama hiyo pia ilifanywa kwa cheti chake cha shahada kutoka chuo kikuu cha Jomo Kenyatta ambao pia walipuuzilia mbali stakabadhi hiyo.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke