Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Asilimia 20 ya watu nchini Nigeria wamepoteza kazi chanzo ni COVID-19

Unempy Asilimia 20 ya watu nchini Nigeria wamepoteza kazi kisa UVIKO-19

Wed, 22 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la kimataifa la Maendeleo (UNDP) pamoja na Ofisi ya Taifa ya Takwimu Nigeria (NBS) zimesema kuwa asilimia 20 ya wafanyakazi nchini humo wamepoteza kazi zao kufuatia kuibuka kwa ugonjwa wa UVIKO-19 katika mwaka 2020.

Mashirika yote haya mawili yametoa ripoti inayohusu madhara ya UVIKO-19 katika biashara nchini humo na data za pande zote zimeonesha asilimia hizo za watu kupoteza ajira zao katika kipindi hicho.

Ripoti zote zimemulika upungufu wa makusanyo ya kodi kitaifa yaliyosababishwa na watu wengi kupoteza kazi katika kipindi cha mlipuko wa ugonjwa huo.

Aidha ripoti hizo zilifanya mahojiano ya kina na wafanyabiashra wapatao 3,000 kutoka sekta binafsi na serikali ambao kwa ukubwa wanachangia pato la taifa nchini humo.

Ripoti hiyo imesema kuwa asilimia 81 ya kampuni kubwa zilifanyiwa mahojiano zimekiri kuporomoka kiuchumi huku aslimia 73 zikiwa zinakabiliwa na changamoto zilizotokana na madhara ya UVIKO-19.

Ripoti hiyo imeangazia pia Sekta ya habari ambayo imeporomoka kwa asilimia 44 tangu mlipuko huo utokee.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live