Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ashitakiwa kwa kushindwa kulipa Bili Hotelini alipokaa kumsumbubiri Mpenzi wake

Nyundo Ashitakiwa kwa kushindwa kulipa Bili Hotelini alipokaa kumsumbubiri Mpenzi wake

Sat, 13 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamume mmoja aliyekaa katika hoteli moja ya kifahari jijini Nairobi Nchini Kenya kwa siku 12 akimsubiri mpenzi wake washerehekee sikukuu ya Mwaka Mpya 2024 ameshtakiwa kwa kushindwa kulipa bili ya KSh466,965. (sawa na Shilingi ya Tanzania Mil. 7,421,637)

Kwa sasa hivi makazi ya Bw Leavan Namayi Lubanga kutoka Kaunti ya Homa Bay yatakuwa ni gereza la Industrial Area alipopelekwa kuzuiliwa akisubiri kesi aliyoshtakiwa isikilizwe na kuamuliwa.

Bw Lubanga alitiwa nguvuni na polisi mnamo Januari 11, 2024, kutoka hoteli ya Pan Pacific iliyoko eneo la Westlands, Nairobi baada ya kushindwa kulipa bili hiyo ya KSh 466,965

“Mheshimiwa nilidanganywa na mwanamke nimsubiri katika hoteli ya Pan Pacific lakini hakutokea. Nilimsubiri kwa siku 12. Nimeshindwa kulipa bili ambayo inajumuisha mlo, malazi na vileo,” Bw Lubanga alimweleza hakimu mwandamizi Gilbert Shikwe.

Kwako mkasa upi ulikutokea maishani ulimuhusisha mwanamke?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live