Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arteta ataja benchi la ufundi Arsenal

89983 Mikel+pic Arteta ataja benchi la ufundi Arsenal

Fri, 27 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

LONDON, ENGLAND. MIKEL Arteta ametaja watu atakaokuwa nao kwenye benchi lake la ufundi na amembakiza Freddie Ljungberg akiendelea kuwa msaidizi wake kwenye kikosi hicho cha Arsenal. Kiungo huyo wa pembeni wa zamani wa Arsenal, Ljungberg aliisimamia timu hiyo katika mechi sita akiwa kocha wa muda baada ya  Unai Emery kufutwa kazi kutokana na timu kufanya hovyo na kuvuna matokeo mabaya. Ljungberg alishinda mechi moja tu, 3-1 alipowachapa West Ham United  na mechi yake ya mwisho ilimalizika kwa sare ya bila kufungana dhidi ya Everton Jumamosi iliyopita. Arteta alikuwa jukwaani Goodison Park kutazama mechi hiyo sambamba na mkurugenzi wa ufundi, Edu na Steve Round, ambaye atakuwa kocha msaidizi. Round alikuwa kocha wa Middlesbrough, Newcastle United, Everton, Manchester United na England na alikuwa mkurugenzi wa soka katika klabu ya Aston Villa. Kwenye orodha ya wasaidizi watatu, mwingine ni Albert Stuivenberg, ambaye aliwahi kuwa msaidizi wa Louis van Gaal huko Old Trafford. Arteta alisema: "Nimefurahi kuwa na kundi hilo la makocha wenye vipaji. Kutakuwa na mchanganyiko wa wazoefu na wenye mawazo mapya. Pamoja na vipaji hivi vilivyopo hapa, tunaamini tutakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuirudisha timu kwenye makali yake ya ushindi."

Chanzo: mwananchi.co.tz