Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal yamvutia kasi winga Ajax Amsterdam

90931 Pic+arsenal Arsenal yamvutia kasi winga Ajax Amsterdam

Mon, 6 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

London, England. Arsenal imefungua milango ya kumsajili winga wa Ajax Amsterdam Hakim Ziyech katika usajili wa dirisha dogo mwezi huu.

Ziyech ameitaka klabu hiyo kumpa ruksa ya kuondoka baada ya klabu za Ulaya kumtupia ndoano.

Hata hivyo, winga huyo ataondoka Ajax ikiwa itavuna Pauni43 milioni inazotaka za kumuuza mwezi huu.

Kiwango cha mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi kimekuwa gumzo kwa idadi kubwa ya klabu za Ulaya zinazotaka saini yake.

Winga huyo mwenye miaka 26 alianza kujiweka sokoni baada ya kucheza kwa kiwango bora katika Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo Ajax ilicheza nusu fainali msimu uliopita.

Arsenal italazimika kuingia vitani kuwania saini ya nyota huyo ambaye anawindwa na Tottenham Hotspurs.

Mchezaji huyo amecheza mechi 104 na amefunga mabao 38 tangu alipojiunga na klabu hiyo akitokea Twente mwaka 2016.

Chanzo: mwananchi.co.tz