Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aplikesheni ya biashara za mipakani yazinduliwa Somalia

Somali App ya biashara za mipakani yazinduliwa Somalia

Fri, 27 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Somalia imeanzisha mfumo wa kutoa taarifa za kibiashara kupitia app ili kuziwezesha biashara zake kuvuka mipaka na kuwapa wafanyabishara fursa ya uwazi na mazingira mazuri ya kibiashara.

App hiyo ilizinduliwa mapema siku ya jumatano ikiwa ni moja ya hatua ya hivi karibuni ya kuboresha biashara na kuvuka mipaka itayoiwezesha Somalia kukutana na Shirika la Biashara Ulimwenguni (WTO) kwa kufuata makubaliano ya Mkataba wa Uwezeshaji Biashara.

Waziri wa Viwanda na Biashara Abdulkadir Sharif Shekhuna amesema app hiyo ambayo itakuwa chanzo cha habari zote za biashara zinazofanyika katika mipaka yake itapunguza gharama na kurahisisha taratibu za ufanyaji biashara kwa waingizaji na wauzaji wa somalia.

"Kwa kuzindua App ya taarifa za biashara Somalia, tuna matuamaini kwamba wafanyabiashara watatumia nyenzo hii muhimu kupata habari muhimu ili kufanikisha shughuli za kuagiza na kuuza nje" amesema Waziri Sharif.

Kwa sasa zaidi ya sheria 90, kanuni, taratibu za biashara na hatua nyingine muhimu zinazohusiana na biashara kutoka kwa mawakala zaidi ya dazeni zinaweza kupatikana mtandaoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live