Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aomba talaka kwa mwanamke waliyekutana Facebook kisa kunyimwa unyumba

0fgjhs34gu8oflgq2g Aomba talaka kwa mwanamke waliyekutana Facebook kisa kunyimwa unyumba

Wed, 25 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mwanamume mmoja huko kaunti ya Nakuru ameomba kumtaliki mkewe ambaye alisema amemnyima tendo la ndoa na kwamba aligundua kuwa yeye ni msagaji.

Jamaa amesema mwanamke huyo baadaye alimfichulia kwamba yeye huvutiwa na wanawakeAliiambia korti wakati walimuoa mwanamke huyo walijamiiana baada ya miezi minane baada ya harusi

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 30 amesema anataka kumtaliki mkewe ambaye alimuoa 2016 kwa sababu ya kumnyima tendo la ndoa

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 30 aliyetambuliwa kama FJO amesema alikutana na mkewe aliyejulikana kama PNM kwenye Facebook mnamo 2015 na Aprili 2016, wawili hao walifunga pingu za maisha.

Hata hivyo, penzi ambalo FJO alidhani litampa raha liligeuka kuwa shubiri baada ya mwanamume huyo kugundua hivi karibu dada huyo amepoteza hamu ya kujamiiana naye, The Standard iliripoti.

Katika stakabadhi za mahakamani, jamaa alimwambia hakimu wa Nakuru Yvonne Khatambi, kwamba PNM alikataa katakata kujamiiana naye baada ya harusi. Alikubali tu kushiriki penzi naye miezi minane baadaye.



Mlalamisjhi ambaye ana mtoto wa kike na mkewe, alisema penzi lao liliingia doa baada ya kudorora kwa mawasiliano baina yao na kukosa kushiriki penzi.

Baba huyo wa mtoto mmoja alisema baada ya muda kusonga, mwanamke huyo alimfichulia dadake na wifi kwamba anavutiwa tu na wanawake.

"Mshtakiwa alimfichulia dadangu na wifi kwamba anavutiwa na wanawake. Ni wakati huo pia alifichua kwamba yeye ni msagaji," alidokeza.

Alisema kwamba ametafuta msaada kutoka kwa familia na hata ushauri wa wataalamu ili kuisimamisha ndoa yake lakini juhudi zake zimeambulia patupu.

FJO alimshutumu mkewe kwa kumnyima asali pasi na kumpa sababu za kuridhisha.

Mwanamke huyo bado hajasema lolote kuhusiana na kesi hiyo.

Hakimu atatoa uamuzi wake kuhusiana na kesi hiyo Septemba 3.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke