Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aokoa maisha ya mumewe baada ya kumpokonya jambazi bunduki

019f8b05ea51e7c7 Aokoa maisha ya mumewe baada ya kumpokonya jambazi bunduki

Tue, 10 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Everline Barasa alichukua hatua ya haraka ya kuiokoa familia yake ambayo ilikuwa inakodolea kifo machoMama huyo kutoka kaunti ya Trans Nzoia alimtega jangili huyo kwa kutumia miguu na kumuangusha chini kabla ya kumpokonya bunduki ya aina ya AK47Mumewe alikuwa amelala kwenye kiti wakati jangili huyo alivamia boma lake na kuitisha KSh 200,000Mwanamke jasiri kutoka kaunti ya Trans Nzoia ameiokoa familia yake kutoka mikononi mwa jangili aliyekuwa amejihami ambaye alivamia boma lake Jumapili, Agosti 8.

Everline Barasa mwenye umri wa miaka 51 alisema jangili huyo alivamia boma lake katika kijiji cha Kaptegaa eneo la Endebess saa tatu usiku na kuitisha KSh 200,000 ambazo walikuwa wamepokea baada ya kuuza kipande chao cha ardhi.

Kulingana na ripoti ya The Standard, jangili huyo alimtishia maisha na bunduki hiyo akimshurutisha kumpa hela hizo naye akapiga magoti kumsihi mshukiwa asimdhuru yeyote katika familia yake.

Mumewe ambaye alikuwa amelala kwenye kiti aligutushwa na purukushani hiyo na wakati Barasa alipomuona akiinuka wazo lilimjia kukabiliana na jambazi huyo.



Read also

Afisa wa Polisi Afariki Dunia Baada ya Kujiteketeza Moto

Mara moja alimrukia jangili huyo aliyekuwa amezubaa akamwangusha sakafuni kisha akafanikiwa kumpokonya bunduki aliyokuwa amejihami nayo.

Mhushikiwa huyo aliponaswa na kuhojiwa alikiri kwamba bunduki hiyo ilikuwa ya mmoja wa maafisa wa polisi ambaye alimlipa kutekeleza uhalifu huo.

Mshukiwa huyo aidha alidai kwamba alikuwa na mwenzake walipoingia katika boma hilo lakini baadaye alihepa wakati njama yao ilipotibuka.

Aliokolewa kutoka mikononi mwa wanakijiji ambao walikuwa na hamaki baada ya mzee wa kijiji kuwaarifu maafisa wa polisi nao wakafika kwa haraka.

Polisi wameanzisha uchunguzi kuhusiana na kisa hicho.

Kwingineko, polisi huko Machakos wameanzisha uchunguzi baada ya majangili watatu kuvamia benki ya Equity eneo la Matuu wiki chache zilizopita.

Kulingana na polisi, watatu hao walivamia taasisi hiyo Jumanne, Julai 27 baada ya kujifanya walikuwa wateja.

Washukiwa hao walimpokonya polisi aliyekuwa akilinda lango la benki hiyo bunduki yake ya aina ya AK47 kabla ya kuingia ndani ya benki hiyo kutekeleza uhalifu.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.



Read also

Murang'a: Polisi Wachangisha Pesa na Kumsaidia Msichana Maskini Kujiunga na Kidato cha Kwanza

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke