Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anusurika kifo baada ya kutobolewa shingo na samaki

Anusurika kifo baada ya kutobolewa shingo na samaki

Mon, 27 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Samaki ni kitoweo muhimu kwa afya ya binadamu kuna aina ya samaki wanaweza kuwa na hatari kwa binadamu.

Uthibitisho wa hilo umetokea hivi karibuni nchini Indonesia, ambapo Muhammad Idul amenusurika kupoteza maisha baada ya kutobolewa na samaki aitwaye Ngarara.

Idul (16) alikuwa kwenye shughuli za uvuvi baharini ndipo ghafla alipotokea samaki huyo na kumtoboa shingoni.

Jeraha alilopata Muhammad limemfanya kuwa maarufu baada ya picha za samaki aliyemtoboa shingoni kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuonekana kote ulimwenguni. 

Akizungumza na BBC Indonesia, siku tano baada ya kutokea kwa tukio hilo, anasema kwamba walikuwa wamepanga kuvua samaki usiku akiwa pamoja na rafiki wake wa shuleni, Sardi.

"Mashua ya Sardi ilitangulia na mimi nikamfuata kwa kutumia mashua nyingine, baada ya muda Sardi akawasha taa, inaonekana ngarara hawezi kuhimili mwanga ndipo alipotoka kwenye maji na kunitoboa shingo yangu.”

Pia Soma

Advertisement
Baada ya hapo Idul alianguka kando ya mashua giza likiwa limetanda kila sehemu. Samaki huyo mrefu, mwembamba na mwenye taya kali akamuuma shingoni, chini tu ya kidevu hadi kwenye fuvu lake. 

Amesema alimshika samaki huyo kwa nguvu akitumai kwamba hata fanya maafa zaidi katika jeraha alilopata. 

"Nilimuomba Sardi usaidizi na yeye akanishauri nisijaribu kumtoa samaki kwa sababu ningetoa damu nyingi," amesema.

Idul alipelekwa hospitali ya jirani akiwa na samaki huyo shingoni lakini baada ya kufika hospitalini, madaktari walifanikiwa kukata mwili wa samaki lakini wakashindwa kutoa mdomo wake uliotoboa shingoni kwa sababu ya ukosefu wa vifaa stahiki. 

Safari ya takribani saa moja na nusu ilianza kuifikia hospitali kubwa ambako madaktari bingwa watano waliingia kwenye upasuaji wa kumuondoa samaki huyo kazi iliyodumu kwa saa moja.

Chanzo: mwananchi.co.tz