Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Angola yavunja rekodi idadi ya vifo ajali za barabarani

Ajali Cd6cbdd73ce Angola yavunja rekodi idadi ya vifo ajali za barabarani

Tue, 21 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ajali za barabarani zimesababisha karibu watu 15,000 kupoteza maisha nchini Angola katika kipindi cha baina ya mwezi Januari hadi Oktoba 2023.

Makamu wa Rais wa Angola, Esperanca da Costa amenukuliwa na vyombo vya habari vya ndani ya Angola akithibitisha habari hiyo na kusema kwenye ujumbe wake kuhusu Siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani na kuongeza kuwa, serikali ya Luanda inaangalia kwa wasiwasi mkubwa maafa ya ajali hizo hasa kwa mwaka huu ambapo ajali na vifo vimeongezeka mno kutokana na ajali za barabarani.

Katika taarifa yake, Makamu wa Rais wa Angola amesema kuwa, kuanzia Januari hadi Oktoba, kumetokea ajali 12,069 za barabarani, majeruhi 2,607, na vifo 14,950 kote nchini Angola. Amesema, hali hiyio inatisha na inazidi kuua watu, kuhangaisha familia na kumtia kwenye majombo kila mtu.

Siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani ilipasishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2005. Huadhimishwa katika Jumapili ya tatu ya mwezi Novemba kila mwaka. Ajali mbaya ya Februari 11, 2021, Fort Worth, Texas Marekani iliyojumuisha magari zaidi ya 100

Kupanda kwa kasi vifo vya ajali za barabarani kumepiga kengele ya hatari katika nchi nzima ya Angola kuhusu wajibu wa kuboreshwa sheria kali za usalama wa barabarani.

Serikali ya Luanda hivi sasa iko kwenye mashinikizo makubwa ya kusaka masuluhisho madhubuti ya kupunguza wimbi la ajali za barabarani.

Kiwango hicho kikubwa cha maafa ya barabarani kimeibua mijadala ya wazi juu ya wajibu wa kuimarishwa miundombinu, utekelezaji mkali wa sheria za barabarani, elimu ya kina kwa madereva, na uwekaji wa viwango vikali vya usalama wa magari kabla hayajaingia barabarani.

Pamoja na kiwango hicho kikubwa cha ajali za barabarani nchini Angola, lakini miji kama ya California na Texas ya Marekani ndiyo inayoongoza kwa maafa na ajali nyingi za barabarani duniani. Tarehe 11 Februari 2021, kulitokea ajali mbaya ya barabara katika barabara kuu wa Fort Worth huko Texas Marekani iliyojumuisha magari zaidi ya 100.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live