Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Angola yajiondoa OPEC

Mafuta Mjadala Angola yajiondoa OPEC

Fri, 22 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Angola imetangaza kujiondoa katika Shirika la Wazalishaji wa Mafuta la OPEC kutokana na mzozo wa mgawo wa pato unaendelea

Hatua ya Angola inafuatia uamuzi wa mwezi uliopita wa shirika hilo lenye wanachama 13 na mataifa 10 washirika kupunguza zaidi uzalishaji wa mafuta mnamo 2024 ili kuongeza bei ya kimataifa

Kwa sasa Angola inazalisha takriban mapipa milioni 1.1 kwa siku, kati ya milioni 30 kutoka OPEC nzima

Taarifa kutoka kwenye Umoja huo zinaelezwa kuwa mgogoro umeanza baada ya Bei ya mafuta kushuka kwa baadhi ya maeneo, huku bei ya Brent ikipungua zaidi ya $1 hadi $78.5 kwa pipa

Uamuzi wa Angola wa kujiondoa kwenye OPEC umetolewa katika mkutano wa Baraza la Mawaziri uliofanyika Alhamisi ya wiki hii

"Tunahisi kwamba kwa wakati huu Angola hainufaiki chochote kwa kubaki katika shirika na, katika kulinda maslahi yake, imeamua kuondoka" -Waziri wa Rasilimali Madini na Petroli, Diamantino Azevedo

"Kama tungebakia OPEC Angola ingelazimika kupunguza uzalishaji, na hii inakwenda kinyume na sera yetu ya kuepuka kushuka na kuheshimu mikataba" -Azevedo

Waziri huyo ameongeza kuwa uamuzi huo haukuchukuliwa kirahisi kwa kuwa Angola na Nigeria ni wauzaji wakubwa wa mafuta katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara

Angola ina hifadhi kubwa ya madini na petroli, na uchumi wake ni miongoni mwa unaokuwa kwa kasi zaidi duniani lakini ukuaji wa uchumi hauko sawa kwa uwiano kwa kuwa sehemu kubwa ya utajiri wake wa mafuta upo katika jimbo lake tofauti la Cabinda, ambapo mzozo wa miongo kadhaa wa kujitenga umeibuka

Angola ambayo imekuwa mwanachama wa OPEC kwa miaka 16 sio nchi ya kwanza kuondoka kwenye shirika hilo kwa kuwa huko nyuma Mataifa kadhaa kama vile Ecuador, Indonesia na Qatar zote zimefanya maamuzi ya aina yote

OPEC ni kundi la wazalishaji wa mafuta ambalo huamua ni kiasi gani cha mafuta ghafi ya kuuza kwenye soko la dunia, pamoja na kundi lililopanuliwa liitwalo OPEC+

Chanzo: www.tanzaniaweb.live