Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Angola waanza upigaji kura Uchaguzi Mkuu

Kuraaa.png Angola waanza upigaji kura Uchaguzi Mkuu

Wed, 24 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu nchini Angola wanapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa rais ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkali tangu uhuru wake mwaka 1975.

Rais João Lourenço wa chama tawala cha MPLA anakabiliana na Adalberto Costa Júnior, kiongozi wa kundi lililokuwa la waasi na kubadilika kuwa upinzani la Unita.

MPLA, chama ambacho kimekuwa madarakani kwa zaidi ya miongo minne, kimekosolewa kwa kutokabiliana na viwango vya juu vya mfumuko wa bei, umaskini na ukosefu wa ajira.

Rais Lourenço ameahidi kufanyia mageuzi uchumi wa Angola unaotokana na mafuta lakini waandishi wa habari wanasema wapiga kura wengi huenda wasimwamini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live