Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Angola, Senegal zasifiwa kutoa $2.5m kwa vikosi vya Afrika Mashariki

Angola, Senegal Zasifiwa Kutoa $2.5m Kwa Vikosi Vya Afrika Mashariki Angola, Senegal zasifiwa kutoa $2.5m kwa vikosi vya Afrika Mashariki

Wed, 28 Jun 2023 Chanzo: Bbc

Katika mkutano wa kurejesha amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, uliowaleta pamoja viongozi wa nchi za Kati, Mashariki, Kusini mwa Afrika, Umoja wa Afrika, na Umoja wa Mataifa, nchi za Angola, Gabon, na Senegal zilisifiwa.

Ilikuwa ni baada ya Angola na Senegal kutoa dola milioni moja kila moja, na Gabon pia kujitolea kutoa dola 500,000, ili kusaidia shughuli za wanajeshi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotumwa DRC.

Nchi za Afrika mara nyingi zinakosolewa kwa kushindwa kutatua matatizo ya kifedha zenyewe na kusubiri msaada kutoka kwa mashirika kama vile Umoja wa Ulaya na nchi Tajiri.

Tangazo la Umoja wa Afrika la mkutano huo wa Jumanne uliofanyika Luanda, Angola linasema kwamba umoja huo unaomba "nchi nyingine za Umoja wa Afrika kutoa msaada wa kifedha kwa ajili ya mipango ya amani barani Afrika".

Je, mkutano huu uliafiki nini kingine?

Mkutano huu wa kwanza wa aina yake uliitishwa na Azali Assoumani, Rais wa Visiwa vya Comoro na mkuu wa Umoja wa Afrika, na mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat.

Ulihudhuriwa na marais João Lourenço wa Angola, Félix Tshisekedi wa DR Congo, Évariste Ndayishimiye wa Burundi, Ali Bongo Ondimba wa Gabon, Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe, na wawakilishi wa Rwanda, Namibia, na Uhuru Kenyatta, mpatanishi katika suala hilo. ya Kongo.

Mkutano huo ulishukuru kwamba Jumuiya ya Mataifa ya Afrika ya Kati ECCAS, inayoongozwa na Rais Bongo - sasa pia iko tayari kusaidia kurejesha amani mashariki mwa Kongo.

Baraza hilo liliomba "makundi yote yenye silaha kurudi nyuma, haswa M23, pamoja na ADF na FDLR", likiwataka M23 "kujiondoa kutoka kwa maeneo yote ambayo imechukua bila kuchelewa".

Washiriki hao walipongeza hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya mahali ambapo wapiganaji hao wa M23 waliopokonywa silaha watahamishiwa.

M23, hata hivyo, inasema kwamba haitaweka chini silaha zake ikiwa serikali ya Kinshasa haitakubali kufanya mazungumzo nao, kitu ambacho serikali ya Kinshasa ilisema hakiwezekani.

Mkutano huu ulianzisha "jukwaa la vitendo" la kuongoza juhudi za kurejesha amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambalo linaleta pamoja nchi hizi zote, Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa, kufuatilia hatua zote ambazo zimeidhinishwa.

Washiriki waliamua kuwa mkutano wa pili wa aina hiyo utafanyika mjini Bujumbura nchini Burundi.

Chanzo: Bbc