Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anayetuhumiwa kuwa daktari wa uongo anaswa akiomba rushwa

Anayetuhumiwa Kuwa Daktari Wa Uongo Anaswa Akiomba Rushwa Anayetuhumiwa kuwa daktari wa uongo anaswa akiomba rushwa

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Idara ya afya ya jimbo la Gauteng nchini Afrika Kusini imewaonya wakaazi kutowalipa wafanyakazi wa afya moja kwa moja baada ya jaribio la daktari wa uongo kuomba hongo katika hospitali nchini humo.

Mwanamke huyo, ambaye alikuwa amevaa vazi la buluu lenye jina "Dr Zulu" lililoandikwa juu ya kifua, anadaiwa kumuomba msindikizaji wa mgonjwa katika Hospitali ya Chris Hani Baragwanath, randi 700 (dola za kimarekani 36) ili apewe msaada.

Msindikizaji huyo alianza kupata shaka pale mwanamke huyo ambaye hajatajwa jina lake, aliposema wakutane kwenye lango la waingia kwa miguu ili kufanya malipo hayo.

Lakini hakuweza kutoa stakabadhi zake za kazi, na baadaye alikamatwa. Mwanamke huyo bado hajazungumza juu ya tukio hilo.

Watu wanaojifanya kuwa matabibu wamekuwa kero kubwa nchini Afrika Kusini, wizara ya afya ilisema mwaka jana kuwa zaidi ya watu 120 walikamatwa wakijifanya matatibu katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Chanzo: Bbc