Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anaswa akiuza sambusa za nyama ya mbwa

Mbwa Sambusa Anaswa akiuza sambusa za nyama ya mbwa

Thu, 9 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi nchini Kenya wamemkamata mwanaume mmoja Ndirangu Wahome katika kaunti ya Nyandarua kwa tuhuma za kuwauzia watu sambusa za nyama ya mbwa bila wao kujua.

Wananchi wa eneo hilo wanasema  kwa muda mrefu wamekuwa wakila vitafunwa hivyo wanavyodai vilikuwa vitamu na ladha tofauti bila kujua kuwa ndani yake sio nyama ya kawaida inayotumika.

Ndirangu Wahome alikamatwa akiuza nyama iliyokaangwa kwenye chungu cha moto katika mji wa Wanjohi baada ya wananchi kutoa taarifa polisi kuhusu wasiwasi wao.

Polisi wanasema kichwa cha mbwa aliyechinjwa pamoja na kisu vilipatikana katika nyumba ya mtuhumiwa huyo vikiwa pamoja na chungu maalum kinachodaiwa kufanya kazi ya kuchemsha nyama hiyo

Aidha pia polisi wamemkuta akiwa na mitego kadhaa anayoitumia kunasa mbwa mitaani na kuwahifadhi nyumbani kwake tayari kwa ajili ya kuuza  

Chanzo: www.tanzaniaweb.live