Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amuua mkewe kisa kapokea simu usiku

Image1170x530cropped Amuua mkewe kisa kapokea simu usiku

Wed, 22 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume mmoja kutoka kaunti ya Kilifi nchini Kenya amehusishwa na mauaji ya mkewe kisa kikiwa ni kupokea simu na sasa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Mtwapa.

Mwanaume huyo ambaye ni dereva wa lori anadaiwa kurejea kutoka safarini na kufanya kitendo hicho cha kinyama baada ya mkewe kupokea simu majira ya saa sita usiku.

Ripoti ya NTV ilionyesha kuwa Lulu Ibrahim mwenye umri wa miaka 29 ambaye alikuwa mama wa watoto sita alikata roho kutokana na majeraha mabaya aliyopata.

Ndugu zake walishindwa kustahimili uchungu wao walipoupokea mwili wa jamaa yao na kulaani tukio hilo wakijutia kutokuwa na imani kubwa kati ya mume na mkewe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live