Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amuua Mwenzake Kisa Nauli ya Bodaboda

BODABODA.png Bodaboda

Thu, 21 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KWELI dunia ina mambo.... Jeshi la Polisi nchini Kenya, Jeshi la Polisi ncini Kenya wanamshikilia mshukiwa wa mauaji ambaye aanadaiwa kumdunga swahiba wake kisu shingoni na kumuua papo hapo, baada ya kutofautiana.

Mshukiwa huyo Daniel Waithera, 25, alimuua rafiki yake Michael Mukami, 21, kufuatia mvutano kuhusu ni nani anayetakiwa kulipa nauli baada ya kubebwa na pikipiki.

Kulingana na mwendeshaji wa bobaboda nhini humo, Stephen Mwango, aliwabeba wawili hao majira ya saa 11:30 asubuhi kutoka Soko la Gikambura, Kikuyu katika Kaunti ya Kiambu.

Hata hivyo, walipofika Muthangari, abiria hao wawili walianza kuvutana kuhusu ni nani aliyestahili kulipa nauli. Kisha mshukiwa aliingia nyumbani kwake na kurejea na kisu chenye ncha kali.

Punde si punde, alimdunga kisu marehemu kwenye upande wa kushoto wa shingo lake na kisha kutoroka akimuwacha maiti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live