Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amnesty yaishtumu serikali ya DR Congo kwa kuwafurusha watu migoni

Amnesty Yaishtumu Serikali Ya DR Congo Kwa Kuwafurusha Watu Migoni Amnesty yaishtumu serikali ya DR Congo kwa kuwafurusha watu migoni

Tue, 12 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Amnesty International imesema Jumanne kwamba upanuzi wa migodi ya madini ya shaba na cobalt katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yenye utajiri wa madini umesababisha kufukuzwa kwa lazima na msururu wa ukiukwaji wa haki.

Taifa hilo la Afrika ya kati lina akiba kubwa zaidi duniani ya cobalt, chuma kinachoonekana kuwa muhimu kwa nishati mbadala kwa sababu ya matumizi yake katika betri za magari ya umeme.

DRC pia ni mzalishaji mkuu barani Afrika wa shaba, chuma kingine cha betri.

Katika ripoti ya kurasa 98, shirika la Amnesty na jingine la kutetea haki za nchini Congo IBGDH liligundua kuwa jamii ndani na karibu na mji wa madini wa Kolwezi, kusini mashariki mwa DRC, walikuwa wamefurushwa kwa nguvu au kutishiwa kuondoka katika makazi yao ili kupisha upanuzi wa migodi.

"Watu wanaoishi katika eneo hili wanapaswa kufaidika kutokana na ukuaji wa uchimbaji madini. Badala yake, wengi wanalazimishwa kutoka katika makazi na mashamba yao," ilisema ripoti hiyo.

Kulingana na mahojiano na watu 133, ushahidi wa hali halisi na picha za satelaiti, ripoti ilichambua athari za miradi minne ya uchimbaji madini katika eneo hilo.

Chanzo: Bbc