Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amnesty International yataka kusitishwa mashambulizi dhidi ya raia DRC

Drc Amnestyyyyy Amnesty International yataka kusitishwa mashambulizi dhidi ya raia DRC

Wed, 21 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International, limetoa wito Jumanne wa kusitishwa mara moja "mashambulizi ya makusudi na ya kiholela dhidi ya raia" katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Taarifa ya shirika hilo imesema, hujuma na mashambulio dhidi ya raia yanapaswa kusitishwa wakati wa mapigano kati ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na wasaidizi wake na jeshi la Rwanda na waasi wa M23 karibu na Goma, mashariki mwa DRC.

Baada ya miezi kadhaa ya utulivu, mapigano makali yalianza tena mwezi wa Januari karibu na Goma, makao makuu ya jimbo la Kivu Kaskazini na kusababisha vifo vya takriban raia 35" na "mamia kujeruhiwa", Tigere Chagutah, mkurugenzi wa Amnesty International katika kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, amesema katika taarifa yake kwamba:

"Maelfu ya raia kwa mara nyingine wamenaswa majumbani na katika majengo mengine kutokana na mapigano na wanahitaji sana msaada wa kibinadamu," amesisitiza, akibaini kwamba leo maelfu ya watu wamejazana ndani na karibu na Goma", baada ya kukimbia mapigano. Raia katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameendelea kuyakimbia makazi yao kutokana na kuibuka machafukko mapya katikak maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo

Mapigano bado yalikuwa yakiendelea siku ya Jumanne karibu na Bweremana, yapata kilomita kumi na tano magharibi mwa Goma, kulingana na wakaazi na mashirika ya kiraia ya eneo hilo yaliyohojiwa kwa njia ya simu.

Maelfu ya watu waliokimbia makazi yao wanaishi katika kambi zisizo salama kiafya mashariki mwa nchi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutokana na mzozo kati ya waasi na jeshi la nchi hiyo.

Mwezi uliopita wa Januari Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo lilitangaza kuanzisha operesheni ya pamoja na wanajeshi wa kikosi cha Jumuiya ya Maendelezo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC dhidi ya waasi wa M23 mashariki mwa nchi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live