Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amezeeka kweli, muonekano mpya wa Miguna wafurahisha Wakenya mitandaoni

5a23dd2b5f0c9988 Amezeeka kweli, muonekano mpya wa Miguna wafurahisha Wakenya mitandaoni

Tue, 18 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Wakili huyo ambaye anaishi mjini Toronto, Canada alipakia picha yake akichapa kazi katika ofisi yake Jumanne, Mei 18

- Picha hiyo ilibainisha kuwa wakili huyo anazeeka vyema

- Baadhi ya wafuasi wake walijaa kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii wakijaribu kumuomba arejee nyumbani

Wakili Mkenya aliyefurushwa nchini Miguna Miguna amepakia picha ya muonekano wake mpya akiwa na ndevu nyeupe.

Wakili huyo ambaye anaishi mjini Toronto, Canada alipakia picha yake akichapa kazi katika ofisi yake Jumanne, Mei 18.

Picha hiyo ilibainisha kuwa wakili huyo anazeeka vyema huku akiambatanisha na ujumbe akisema: "Marathon tulioanza Machi 29, 2021, inakamilika. Viva!"

Baadhi ya wafuasi wake walijaa kwenye kurasa zake za mitandao ya wakiwa na matumaini kuwa atafaulu kurejea nyumbani.

Hii hapa maoni yaoTogom Peter aliandika: "Sasa wewe ni mzee mkubwa. Naona mvi."

Isaac Onjiko alisema: "Napenda muonekano wako mpya. Siku inakuja na bado tuna matumaini. Uwe salama."

Motari Caleb: "Unazeeka Viva!"

Nixon Otieno alisema: "General, muoneknao huo unawasumbua despots Viva!

TUKO.co.ke iliripotia awali namna Miguna alivua kofia yake na hatimaye kuonyesha kiara yake baada ya kuificha kwa miaka.

Miguna alichapisha picha hizo nadra kwenye ukurasa wake wa Facebook mnamo Jumamosi, Julai 1, pengine kukarbisha mwezi mpya.

"Ahadi ilitolewa na sasa imetimizwa. Despots na mizuka wao wamekuwa wakitaka kuona kichwa changu.Hiki hapa. Nasherehekea Siku ya Hezekiah Ochuka Raballa - Agosti 1 - na kujiunga na familia yake kuitisha eneo ambalo alizikwa ili mabaki yake ifukuliwe na kuandaliwa mazishi ya hadhi," aliandika Miguna kwenye ujumbe akiambatanisha picha hizo.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke